Ijumaa, 8 Mei 2020

BREAKING NEWS: AFANDE MASOUD MOHAMMED AMEFARIKI DUNIA GHAFLA LEO AKIWA HOTELINI NA SABABU YA KIFO CHAKE BADO HAIJAFAHAMIKA

MASOUD Mohammed ndio jina lake. Alikuwa akitumikia Jeshi la Polisi Tanzania. Ukitazama katika video hii ana nyota 3 begani, lakini kabla ya Aprili 17 mwaka huu, alikuwa na nyota 2. Aprili 17, alipost hapa instagram kuonesha kwamba amepanda cheo, ndipo tukaona nyota 3.
.
Kupanda cheo itudhihirishie kwamba alikuwa muadilifu na mchapakazi. Lakini pia, hakusahau jukumu lake kwa muumba wake. Alitrend na video hii akighani #Quran. Hivyo ndiyo alivyotumia mtandao.
.
Jana alipost kwenye account yake, akimuomba Mungu atujaalie mwisho mwema. Aliandika "Muislamu safi, ni Yule ambae watu hawapati madhara kutokana na mdomo wake au  mikono yake"  Allah atujaalie mwisho mwema  tusiwe miongoni mwa watu wabaya !" -
Hiyo ndiyo post yake ya mwisho, leo trending news ni kwamba Afande Masoud amefariki. Taarifa za awali zinasema amekutwa nyumbani kwake akiwa ameshaaga dunia.
.
Wengi hawakumfahamu, lakini muda huu wanatiririka kwenye account yake (@masoudtheking) kufahamu alikuwa mtu gani. Wakifika hapo watakutana na ASKARI MUADILIFU, MCHA MUNGU, ALIYETANGAZA MATENDO MEMA. Swali kwetu tuliobaki : Tunatumiaje mitandao, tukiondoka tutaacha alama gani?
.
#InnaliahWainailahRajiun.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni